Yote Huanza Na Mungu

Nawasalimu katika Jina la Yesu, Bwana na mwokozi wa maisha yetu, Neema ya Mungu na Upendo wake Uwe nanyi daima,
Kuelekea katika Tamasha la Vijana, KKKT-DMP Usharika wa Kiluvya, ambalo linatarajia kufanyika tarehe 28/4/2017 lenye ujumbe mkuu " Find Your Purpose " likimaanisha tafuta KUSUDI la maisha yako, Umoja wa vijana kiluvya unapenda kuwaalika walengwa wote wa tamasha hilo kuhudhuria bila kukosa.
Mara nyingi hili swali la kujua kusudi ya maisha yako huwa linawatatiza wengi, na vitabu vingi vimeandika kwa ajili ya kutoa majibu ya hili swali, "nini kusudi la maisha yangu?". Na mara nyingi tunajiuliza maswali mengi kibinafsi kama Je nataka kuwa nani, nifanye nini na maisha yangu? Malengo yangu ni Yapi?
"Kwa kua katika yeye vitu vyote viliumbwa vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, Vinavyoonekana na visivyoonekana, ikiwa ni vitu vya enzi au usultani au enzi, au mamlaka;vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na KWA AJILI YAKE"(Wakolosai 1:16) Hivyo basi kusudi lako katika maisha linaanza na Mungu.
Napenda kuwakaribisha katika Mkesha huu Mkubwa wa kumsifu na kumwabudu Mungu, kwa kutambua kwamba tumeumbwa kwa ajili yake na kusudi la maisha yetu linaanza na Yeye.
Yote Huanza na Mungu


0 comments: